Baada ya sakata la mchezo namba 184 dabi ya Kariakoo kupata ufumbuzi, Wananchi sasa wanaelekeza nguvu zao katika mechi zote tatu zilizobaki ili kuhakikisha wanatetea ubingwa
Kabla ya kumalizana na Simba Juni 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga inahitaji kubeba alama zote sita za mechi mbili zinazofuata
Juni 18 Yanga itashuka dimba la Sokoine mkoani Mbeya kumenyana na Tanzania Prisons katika mechi ambayo alama tatu ni muhimu kwa Wananchi
Yanga kimeendelea kujifua KMC Complex kabla ya safari ya kuelekea mkoani Mbeya





ADVERTISE HERE