Sakata la Yanga na TFF, uwajibikaji uonekane

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2025
Sakata la Yanga na TFF, uwajibikaji uonekane

Moto wa mgogoro kati ya Yanga SC na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaendelea kuwaka kwa kasi, huku sauti za kutaka Rais wa TFF, Wallace Karia ajiuzulu zikipamba moto kutokana na madai mazito ya kutolipwa fedha za ubingwa wa Kombe la FA (CRDB) kwa kipindi cha misimu mitatu.

Yanga wameibuka hadharani na kudai kuwa hawajawahi kulipwa fedha walizopaswa kupata baada ya kutwaa taji hilo kwa misimu mitatu mfululizo, huku madai yao yakiifikia jumla ya zaidi ya Tsh milioni 490. Taarifa yao inaonesha kuwa hata baada ya TFF kukata fedha kwa kigezo cha "madeni", bado wanastahili kulipwa Tsh milioni 226.

TFF, kwa upande wao, walijibu kwa kueleza kuwa wamepokea malipo kutoka kwa CRDB wadhamini wa kombe hilo kiasi cha Tsh milioni 215, lakini fedha hizo hazikufika kwa Yanga kwa kile walichokiita makubaliano ya awali ya kukata madeni ya klabu hiyo moja kwa moja kutoka kwenye zawadi za ushindi.

Hali hii imeibua mjadala mpana mitandaoni, na sauti za mashabiki na wadau mbalimbali wa soka zinasikika kwa nguvu zaidi. Haji Manara, aliyewahi kuwa msemaji wa Yanga, ameibua hoja nzito akihoji kwa nini Karia bado yupo ofisini licha ya kashfa hii.

β€œHuyu bado yupo tu pale Karume? Anangoja nini sasa? Wamekula pesa za sponsor miaka mitatu kwa kisingizio cha madeni kisha bado wapo ofisini tu,” aliandika Manara katika mitandao ya kijamii.

Kinachozidi kuchochea moto ni ukweli kwamba CRDB walitoa tamko kuwa wamekamilisha majukumu yao ya kimkataba kwa kuilipa TFF, hivyo deni liko mikononi mwa Shirikisho hilo. Wakati mashabiki wakitegemea suluhisho la haki, TFF waliita Yanga 'mezani' kwa kile walichokiita uhakiki wa madeni, lakini hali hiyo ikaonekana kama kujaribu kupooza jazba badala ya kutafuta suluhu ya kweli.

Tukumbuke, sakata hili liliibuka kwa nguvu zaidi wakati Yanga walipotishia kutoshiriki fainali ya Kombe la FA msimu huu, kama hawatalipwa fedha zao walizodai kwa msimu uliopita. Hatua hiyo ililazimisha CRDB na TFF kujitokeza kutoa kauli, lakini badala ya kuzima moto hali imezidi kuchafuka.

Je, Karia atapona kwenye hili?

Kwa sasa, shinikizo linaongezeka. TFF inakumbwa na ukakasi wa wazi wa uongozi na uaminifu. Kama kweli Yanga hawajalipwa kwa misimu mitatu, huku TFF wakipokea fedha kutoka kwa mdhamini, basi kuna swali kubwa linalobaki: Fedha hizo zimekwenda wapi?

Kwa vyovyote vile, sakata hili linapaswa kuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa katika usimamizi wa fedha ndani ya taasisi za soka nchini. Uwazi na uwajibikaji lazima vitamalaki, la sivyo taswira ya TFF itaendelea kuchafuka na huenda Karia akawa mhanga mkuu wa presha hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’