Sisi tunaweza kusimamia maslahi yetu - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2025
Sisi tunaweza kusimamia maslahi yetu - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Yanga ni taasisi imara inayojitosheleza kutetea na kusimamia maslahi yake

Kamwe ametoa kauli hiyo baada ya taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba mapema leo ambapo pamoja na mambo mengine, wameitaka Bodi ya ligi kutoa hadharani ripoti iliyopelekea kuahirishwa kwa namba 184 ambao awali ulipangwa kupigwa March 08

Kamwe amesema taarifa ya Simba waliyoitoa leo inaibua maswali zaidi kwa sababu klabu hiyo awali ilitangaza kutocheza mechi yoyote hadi pale waliokwamisha mchezo huo wachukuliwe hatua

Kamwe amewataka watani zake hao wasubiri Juni 15 wakapewe alama za bure uwanja wa Benjamin Mkapa kwani masuala mengine yote ni kati ya Yanga na Bodi ya ligi

Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram, Kamwe ameandika ujumbe huu;

"Katika hili ni bora mngekaa kimya tu. Jamii ya watu wenye Maarifa na Akili timamu, imeshajua UNAFKI wenu.

Mwanzo mlitangaza hamtashiriki Ligi tena mpaka mtakapopewa ripoti ya uchunguzi wa kilichokwamisha Derby, Ila baada ya mchongo wenu mlioset kujibu, mnatoka mbele eti mnataka tena mechi.

Wanafki wakubwa nyie.

Kilichobadilika ni nini? Ni mtu tofauti aliyeandika mwanzo akidai hamchezi Tena mpaka Ripoti itoke na huyu aliyeandika upuuzi wenu Leo?

Au kwa kuwa ile ya mwanzo iliandikwa Usiku sana tuamini mwandishi alishavesha Konyagi za kutosha kichwani akajiandikia msioweza kuyasimamia?

Niwaambie, katika hili la kudai HAKI NA RIPOTI hatuhitaji sapoti yenu. Sisi Tunajimudu na Tunaweza kuyapambania maslahi yetu bila UNAFKI WENU

Nyie tulizeni mshono, ikifika Tarehe mliyoambiwa, pelekeni Timu kachukueni pointi 3 na tangazeni ubingwa.. Mchecheto wa nini kwani? Mnaacha maswali mengi kwa watu kuonyesha mna wasiwasi na Hamjiamini

Sisi Tunasimamia Maslahi ya mpira, Haki itendeke halafu ndio Mechi halali ipangwe. Tunawatamani sana na mnalijua hilo.

Na ni vyema mkajua, mapambano yetu sio kwa ajili ya kubeba Ubingwa mezani. Sisi hatutakuwa Tayari kubeba Ubingwa Mezani bila kumalizana na nyie Uwanjani

Haki ikishatendeka, Tutawatafuta kivyovyote vile ili TUMALIZANE na Tukomeshe Kimdomo chenu

Kwa sasa Tuacheni kidogo tumalize Jambo kubwa lililo mezani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’