Klabu ya Yanga imewasilisha ombi rasmi la kucheza mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, mnamo Juni 22, siku ambayo ligi itahitimishwa kwa mechi mbalimbali kuchezwa kwa wakati mmoja kote nchini.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi, timu mwenyeji inaruhusiwa kuchagua kucheza mechi mbili nje ya uwanja wake wa nyumbani, na Yanga imetumia fursa hiyo kupeleka mechi yake visiwani Zanzibar. Hii ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuimarisha uhusiano wake na mashabiki walioko visiwani pamoja na kujiandaa vizuri kwa majukumu yanayofuata.
Baada ya mchezo wao wa Juni 18 dhidi ya Tanzania Prisons, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea moja kwa moja Zanzibar, ambako kitakaa kwa takribani siku 10.
Mbali na mechi ya mwisho ya ligi, Yanga itacheza pia fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars, ambayo pia itapigwa katika uwanja huo huo wa New Amaan Complex. Hii inafanya uwepo wao visiwani kuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya kuhitimisha msimu kwa mafanikio.
Yanga imedhamiria kutetea mataji yote mawili Ligi Kuu na Kombe la FA, ambayo wameyashikilia kwa misimu mitatu mfululizo