Mtego mwingine kwa Bodi ya Ligi ni huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jun 2025
Mtego mwingine kwa Bodi ya Ligi ni huu

Kuelekea Dabi ya Kariakoo iliyopangwa kupigwa Juni 15, Klabu ya Yanga imeonesha wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa mashabiki wake, kufuatia matukio ya hivi karibuni yanayohusisha vitendo vya vurugu kutoka kwa mashabiki wa timu hasimu, Simba SC.

Katika tamko rasmi lililotolewa na uongozi wa Yanga hivi karibuni, klabu hiyo ililaani vikali mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya mashabiki wao wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) kati ya Simba na RS Berkane, mchezo uliopigwa visiwani Zanzibar wiki iliyopita.

Yanga imetaka mamlaka husika ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahusika wa matukio hayo ambayo imeyataja kuwa ya aibu na yanayokinzana na maadili ya michezo.

Picha na video zilizotapakaa mitandaoni zimeonesha wazi mashabiki wa Yanga wakishambuliwa bila hatia, lakini hadi sasa hakuna tamko lolote kutoka TFF wala Simba SC kulaani au kujibu matukio hayo. Ukimya huo unaongeza hofu na sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Yanga na wanachama wake.

Cha kusikitisha zaidi, matukio ya vurugu yamejirudia hivi karibuni katika mechi ya Ligi Kuu kati ya Simba SC na Singida Black Stars iliyopigwa katika Uwanja wa KMC Complex, ambapo baadhi ya mashabiki wa Simba walihusishwa tena na vitendo vya fujo na uvunjifu wa amani wakiwashambulia wachezaji wa Singida Black Stars

Kutokana na mfululizo huu wa matukio, ni wazi hii ni sababu nyingine ambayo itaifanya Yanga isicheze mchezo namba 184 uliopangwa kupigwa Juni 15 baada ya matukio yaliyojitokeza March 08

Kauli ya Mzee Msumi, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Yanga aliyoitoa juzi imebainisha viashiria vya uvunjifu wa amani ni dhahiri, na kwamba ni muhimu kwa Bodi ya Ligi pamoja na TFF kuchukua hatua za haraka, ikiwa pia ni pomoja na kuweka hadharani ripoti ya uchunguzi baada ya kuahirishwa kwa mechi ya kwanza iliyopaswa kupigwa March 08

Ikumbukwe kuwa mchezo wa awali wa Dabi hiyo uliokuwa umepangwa kufanyika Machi 8 ulishindwa kuchezwa moja ya sababu iliyotajwa na Bodi ya Ligi ikiwa viashiria vya uvunjifu wa amani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’