Keita na Traore kuelekea Jangwani? Yanga yaongeza kasi kuwanasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2025
Keita na Traore kuelekea Jangwani? Yanga yaongeza kasi kuwanasa

Klabu ya Yanga SC inaendelea kusuka kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao huku macho yao yakielekezwa kwa nyota wawili wa kimataifa: Ibrahim Keita wa TP Mazembe na Fily Traore anayeichezea Asswehly ya Libya.

Wawakilishi wa kampuni ya SABABU Sport Management, inayoshughulika na uwakala wa wachezaji, wako nchini kwa lengo la kukamilisha mazungumzo yanayowahusu wachezaji hao.

Ibrahim Keita (23), beki wa kulia raia wa Mauritania anayeitumikia TP Mazembe, anatajwa kuwa chaguo namba moja kuziba pengo la Yao Kouassi, ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti na huenda akakosekana kwa zaidi ya miezi sita.

Keita pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Mauritania, na mkataba wake na TP Mazembe unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Kwa sasa, amegoma kuongeza mkataba mpya, hatua inayoipa Yanga nafasi nzuri ya kumnasa bila gharama kubwa ya uhamisho.

Kwa upande mwingine, Yanga inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji hatari Fily Traore (23), raia wa Mali, ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Libya msimu huu akiwa na mabao 16 akicheza kwa klabu ya Asswehly.

Hapo awali, Traore alihusishwa na Wydad Athletic ya Morocco, lakini dili hilo lilikwama, jambo lililoipa Yanga nafasi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Mali.

Yanga tayari imemuuza kiungo wake mahiri Stephane Aziz Ki, na kuna taarifa kuwa mshambuliaji chipukizi Clement Mzize pia yuko mbioni kuondoka. Vilevile, Kennedy Musonda anatarajiwa kuondoka baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Hali hii inalazimu Yanga kuongeza washambuliaji wapya angalau wawili kuhakikisha safu ya ushambuliaji inabaki imara.

Kwa sasa, klabu hiyo pia imehusishwa na mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah, ambaye naye anaonekana kuwa kwenye rada ya benchi la ufundi la Yanga kama sehemu ya maamuzi mapya ya kuimarisha kikosi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’