Chama kuamua hatma yake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2025
Chama kuamua hatma yake Yanga

Wakati msimu wa ligi kuu ukitarajiwa kufika tamati mwezi ujao, tayari michakato ya usajili inaendelea kwa nyota ambayo mikataba yao inaelekea ukingoni

Uongozi wa Yanga ulianza mapema michakato ya kuhuisha mikataba ya wachezaji ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu

Mpaka sasa wachezaji kama Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Dickson Job tayari wameramba mikataba mipya huku wachezaji wengine kama Khalid Aucho na Clatous Chama mazungumzo yakiwa yanaendelea

Hata hivyo kwa upande wa Chama imeelezwa kiungo huyo wa zamani wa Simba amepewa ya mkataba wa mwaka mmoja ambao thamani yake imezingatia mchango wake katika kikosi cha Yanga msimu huu

Kuna taarifa pia waajiri wake wa zamani Simba wanapambana kutaka kumrejesha kiungo huyo aliyejijengea heshima kubwa katika soka la Tanzania

Katika msimu wake wa kwanza na Yanga, Chama amekuwa na wakati mgumu kupenya katika kikosi cha kwanza mbele ya Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua ambao wamekuwa katika ubora mkubwa

Chama amefunga mabao manne na kutoa asisti mbili katika ligi kuu ya NBC ambazo zaidi ya asilimia 80 ya mechi alizocheza, alitokea bench

Hata hivyo baada ya Aziz Ki kuondoka, pengine ni nafasi yake kurejea katika kikosi cha kwanza lakini pia msimu ujao eneo analocheza linatarajiwa kuwa na ushindani zaidi kwani Yanga inatarajiwa kusajili fundi mwingine kuchukua nafasi ya Aziz Ki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’