Yanga haiachi kitu msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2025
Yanga haiachi kitu msimu huu

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameweka wazi malengo ya kuhakikisha kikosi chake kinatwaa mataji mawili yaliyobaki ili kufunga msimu na mataji manne

Licha ya kutofanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa, Yanga imekuwa na kampeni nzuri katika mashindano ya ndani mpaka sasa

Wananchi kabatini wana mataji mawili ya Ngao ya Jamii na Ligi ya Muungano huku wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC na fainali ya michuano ya kombe la CRDB

Hamdi ambaye tangu akabidhiwe majukumu ya kuinoa Yanga hajapoteza mchezo wowote, ameweka wazi kuwa hawahitaji kufanya makosa katika mechi za mwisho kuhitimisha msimu

"Tunafurahi tunakwenda katika mapumziko tukiwa tunaongoza ligi lakini tuko hatua ya fainali ya kombe la CRDB. Niseme tu, bado hatujakamilisha kazi"

"Mechi za mwisho zina umuhimu wa kipekee na hatupaswi kufanya makosa, tunajua hatma ya kutetea ubingwa iko mikononi mwetu kama hatutafanya makosa tutakuwa mabingwa"

"Ilikuwa muhimu pia kushinda mchezo dhidi ya JKT Tanzania na kutinga fainali ya kombe la FA, tuna nafasi nyingine ya kutetea taji la FA kwa mara nyingine," alisema Hamdi

Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya muda mfupi na watarejea kambini Juni 1 kwa ajili ya mechi za kuhitimisha msimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’