Yanga, Sowah bado kidogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2025
Yanga, Sowah bado kidogo

Klabu ya Yanga SC inaonekana kutopoteza muda katika maandalizi ya msimu ujao wa 2025/2026, baada ya kumuuza kiungo wao nyota Stephane Aziz KI, aliyejiunga na Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa hao wa Tanzania Bara wamepiga hatua kubwa kwa kuhakikisha wanaboresha safu ya ushambuliaji — na jina la Jonathan Sowah limewekwa kwenye mstari wa mbele.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, tayari mazungumzo ya siri baina ya viongozi wa Yanga na mshambuliaji huyo kutoka Ghana yamefanyika na kufikia makubaliano ya awali. Uwezekano ni mkubwa Sowah atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao, akiandaliwa mkataba wa miaka miwili

Sowah, ambaye kwa sasa anachezea Singida Black Stars, amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipojiunga na timu hiyo kupitia dirisha dogo la usajili mwezi Januari. Amecheza mechi 11 na kufunga mabao 11 — takwimu zinazothibitisha uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu.

Yanga, ambao wanaelekea kumuuza mshambuliaji chipukizi Clement Mzize kufuatia mvuto wake kwa vilabu vya Afrika na Ulaya, pia wanatarajia kuachana na Kennedy Musonda ambaye mkataba wake unatarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu. Hii itatoa nafasi ya usajili wa mchezaji wa kigeni kwa ajili ya kumpokea rasmi Sowah.

Inadaiwa kuwa, licha ya Sowah kuwa bado na mkataba na Singida Black Stars, mshambuliaji huyo mwenyewe kipaumbele chake ni kujiunga na Yanga kwani aliwahi kusema kwamba klabu ya Yanga ni 'nyumbani kwake'

Yanga inalenga kuunda safu ya mashambulizi itakayokuwa chini ya Jonathan Sowah na Prince Dube, wakitegemewa kuibeba timu hiyo katika harakati zake za kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’