Msafara wa mashabiki na wanachama wa Yanga unaondoka Makao Makuu Jangwani kuelekea Tanga kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Mkwakwani
Stika za 'HATUCHEZI N'GO' zimetawala katika mabao hayo zaidi ya 30 yanayoelekea Tanga
Yanga imeamua kutumia utaratibu huu kufikisha ujumbe kwa wenye mamlaka kuwa hawako tayari kucheza mechi namba 184 dhidi ya Simba iliyopangwa kupigwa Juni 15
Yanga inaamini mchezo huo ulipaswa kupigwa March 08 lakini kwa makusudi, watani zao Simba wakaamua kuingia mitini kwa sababu zao wenyewe
Bodi ya ligi ilipaswa kusimamia kanuni lakini badala yake 'wakaibeba' Simba na kuahirisha mchezo huo pasipo sababu za msingi
Sasa wameupangia mchezo huo tarehe mpya pasipo kueleza UMMA nini kilipelekea mechi hiyo ikashindwa kufanyika March 08?
Wananchi wanakwenda Tanga na ujumbe wa HATUCHEZI N'GO