Makosa ya safu ya ulinzi katika dakika 15 za kwanza yameigharimu Yanga Princess ikikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa JKT Queens katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake
Baada ya kuingia mabao hayo, vijana wa kocha Edna Lema walikaa sawa na kutoa upinzani kwa JKT Queens ambao ushindi huo umewapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi wakiiondosha Simba Queens katika nafasi hiyo
Yanga Princess imeendelea kusalia nafasi ya tatu ikiwa na alama 33, imebakisha mechi mbili za kumalisha ratiba ambazo matokeo yake hayawezi kuwaondoa katika nafasi hiyo
Wakati Wananchi wakisikitika kupoteza mchezo huo, matokeo hayo yamepeleka kilio kwa watani zao Simba Queens ambao walitamani Yanga Princess ishinde mchezo huo au hata ipate matokeo ya sare
Msimu huu ni kama umemalizika kwa Yanga Princess lakini bila shaka kikosi kimeiva na msimu ujao pengine kitakuwa katika kiwango cha ushindani sawa na JKT Queens na Simba Queens zilizotawala ligi ya Wanawake kwa misimu kadhaa