Yanga Princess kumenyana na JKT Queens Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2025
Yanga Princess kumenyana na JKT Queens Jumatano

Kesho Jumatano, May 14 Yanga Princess itashuka dimba la Meja Jenerali Isamuhyo kumenyana na JKT Queens katika mechi ya mzunguuko wa 16 ligi kuu ya Wanawake (WPL)

Hii ni mechi ya aina yake kwani matokeo yanaweza kuamua hatma ya ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake msimu huu kati ya Simba Queens na JKT Queens

Kwa lugha rahisi unaweza kusema Simba Queens ambayo jana ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mashujaa Queens inaomba Yanga Princess ipate ushindi au hata kutoka sare na JKT Queens ili waweze kutwaa ubingwa

Yanga Princess ina nafasi finyu ya kutwaa ubingwa msimu huu kwani kama itashinda mechi tatu zilizobaki, itafikisha alama 42 wakat Simba Queens inayoongoza ligi ina alama 41 ikisalia mechi mbili huku JKT Queens inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 38 na mechi tatu mkononi

Mchezo kati ya JKT Queens dhidi ya Yanga Princess awali ulipangwa kupigwa jana lakini ukasogezwa mbele kwa siku mbili hadi siku ya Jumatano

Tangu kuanza kwa duru ya pili ligi kuu ya Wanawake, Yanga Princess imeshinda mechi zote ikiwa ni pamoja na kuwachapa watani zao Simba Queens lakini pia wakiifunga JKT Queens katika michuano maalum ya kuadhimisha siku ya Wanawake na kutwaa ubingwa mkoani Arusha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’