Keita atajwa kurithi mikoba ya Yao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2025
Keita atajwa kurithi mikoba ya Yao

Mashabiki wa Yanga hawajamuona uwanjani beki wao Yao Kouassi, kwa muda sasa akipambana kurudi uwanjani kutoka kwenye majeraha ya nyama za paja, lakini hatua hiyo inawavuruga zaidi mabosi wakiwa na hesabu kali.

Yao, maarufu kwa jina la Jeshi alianza kupona, lakini inaelezwa amepata majanga mengine eneo aliumia awali ambapo huenda akakaa nje kwa muda zaidi.

Yanga inasubiri ripoti ya madaktari wa klabu kufahamu mchezaji huyo atakuwa nje kwa muda gani, lakini nyuma yake kuna hesabu mpya zinapigwa juu ya beki mmoja wa kazi kutoka TP Mazembe ya DR Congo.

Endapo Yao atashindwa kuwahi kurudi licha ya kuonekana anajaribu kuchezea mpira mazoezini, Yanga itamshusha beki Ibrahima Keita, raia wa Mauritania.

Hesabu za Keita na Yanga hazijaanza sasa, kwani beki huyo jina lake kwa mara ya kwanza lilitua Jangwani tangu Kocha Nasredine Nabi anainoa timu hiyo, ambaye alitaka kumsajili kama angebaki kabla ya Julai 17, 2023 kutimka FAR Rabat ya Morocco.

Baada ya Nabi kuondoka, Yanga ikamsajili Yao kuchukua nafasi ya Mkongomani, Djuma Shaban, huku Keita akitua TP Mazembe akitokea Bobigny U19 ya Ufaransa.

"Yao kwa kweli maisha yake msimu huu wa pili si mazuri, amekumbana na janga la majeraha, hivi karibuni tuliona kama amepona, lakini ghafla amerejea tena kwenye majeraha na sidhani kama tutamuona uwanjani tena msimu huu"

"Ilikuwa tumalizane na yeye, lakini tunataka kwanza kupata ripoti kamili juu ya muda gani atakuwa nje halafu tutafanya uamuzi wa kipi kifanyike kwake"

"Hakuna asiyejua uwezo wa Yao akiwa sawa, huyu ni jeshi hasa kama ambavyo mashabiki wanamuita, inatuumiza kwa anayoyapitia lakini ndio soka," mtoa taarifa alinukuliwa na Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
29m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
38m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’