Klabu ya Yanga iko mbioni kumalizana na Lipuli FC kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo Adam Salamba.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amethibitisha juu ya uwepo wa mchakato huo ambapo amesema kwa sasa tayari wameiandikia rasmi barua klabu ya Lipuli ili wamruhusu mchezaji huyo aitumikie Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho inayoendelea hatua ya makundi.
Akiruhusiwa, Salamba ataitumikia Yanga kwenye michuano ya CAF CC pekee na kuendelea kuitumikia Lipuli kwenye michezo ya ligi kuu ya Vodacom hadi mwishoni mwa msimu.
"Tayari tumeshawaandikia barua Lipuli FC kumuomba Adam Salamba kwa ajili ya CAF Confederatins Cup," amesema Mkwasa.
Yanga inaweza kuongeza wachezaji watatu kuimarisha kikosi chake kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE