Mapema leo Bodi ya ligi iliupangia terehe mchezo namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao ulipaswa kupigwa March 08 uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika taarifa ya awali iliyotolewa na Bodi wakati wakitangaza kuahirisha mchezo huo, walieleza kuwepo kwa uchunguzi wa masuala mbalimbali. Miongoni ni masuala ya tishio la kiusalama pia tuhuma za rushwa
Wakati Yanga ilipoandika barua TPLB kuomba hatua kuchukuliwa kwa mujibu wa kanuni walijibiwa kuwa haiwezekani kwa sababu kuna masuala ambayo uchunguzi wake haujakamilika
Kitendo cha kupangia tarehe mchezo huo pasipo kuweka hadharani majibu ya uchunguzi huo kunaibua maswali zaidi
- Imekuwaje ratiba ya mechi imepangwa pasipo majibu ya uchunguzi huo kutolewa? Wadau wataaminije kama sababu zilizotolewa awali zina ukweli?
- Nani alisababisha mechi ya kwanza isichezwe?
- Bodi imechukua hatua gani kwa upande uliopelekea mechi hiyo kutochezwa March 08?
- Nini hatma ya mashabiki ambao walilipa viingilio kushuhudia mchezo huo?
Ni wazi jambo hili bado lina ukakasi mkubwa hasa inapoonekana wenye mamlaka wanataka mechi ichezwe tu pasipo uwajibikaji
ADVERTISE HERE