Hakuna VAR, waamuzi wanaongeza dakika 15 baada ya dakika 90 kweli? Mnadhani hii ni bahati mbaya? wanaelekezwa wafanye hivyo
Kama una umakini fuatilia mechi ambazo timu ile haijapata ushindi baada ya dakika 90, zitaongezwa dakika 10 au zaidi lakini pia ndani ya muda huo wa nyongeza ni lazima wapewe penati au tukio lolote ambao litawasaidia kushinda
Kwa wale 'waliosoma cuba' wanaweza kuelewa kwa nini Mwanasheria wa zamani wa Yanga Simon Patrick alisema vita dhidi ya wahuni sio nyepesi
Hichi kinachofanyika sasa ni 'uhuni' wa kulazimisha timu fulani ishinde hata pale isipostahili
Halafu tunatamba ligi yetu ni namba tano kwa ubora? Haya ni maajabu....!
Hii vita ni ngumu, Wananchi tuwaombee viongozi wetu kwani hayo wanayokutana nayo nyuma ya pazia katika kuipambania Yanga, yatakuwa makubwa
Ni wazi wenye mamlaka wamejipanga kuhakikisha timu yao inachukua ubingwa msimu huu, dalili ni hizi....!