Klabu ya Yanga iko katika mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa klabu ya Singida Black Stars, Joseph Arthur Bada ili kuipata huduma yake kwa msimu ujao
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, imedokeza kuwa mazungumzo hayo yako katika hatua za mwisho, uwezekano wa Bada kutua Yanga ni mkubwa
Bada amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Singida Black Stars akifunga mabao 3 na kutoa asisti 8 katika ligi kuu ya NBC
Yanga imepania kuimarisha eneo lake la kiungo cha ushambuliaji katika mkakati wa kufanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Bada atatua Yanga kama mchezaji mzawa baada ya kubadili uraia wake wa Ivory Coast na kuwa Mtanzania
Kama michakato itakwenda vyema, Yanga huenda ikasajili nyota wawili kutoka Singida BS kwani pamoja nae ni mshambuliaji Jonathan Sowah ambaye tangu atue Singida BS, kwa wastani amefunga katika kila mechi ya ligi aliyocheza akifunga mabao 11 katika mechi 11