Waarabu wamemkomalia Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2025
Waarabu wamemkomalia Aziz Ki

Kuna uwezekano mkubwa klabu ya Yanga itafanya biashara ya maana katika dirisha lijalo la usajili ofa zikimiminika kuwahitaji nyota wa klabu hiyo

Klabu ya Wydad Athletic mara kadhaa imefanya jitihada za kuwasajili Stephane Aziz Ki na Clement Mzize lakini michakato haikufanikiwa kwa sababu ofa yao ilikuwa chini ya mahitaji ambayo Yanga iliweka ili kuwauza wachezaji hao

Hata hivyo taarifa ya ndani ya uongozi wa Yanga imedokeza kuwa klabu za FAR Rabat na Raja CA zimeonyesha kuwa tayari kufikia ofa ambayo Yanga wameitaka ili kumuachia Aziz Ki

Kuna uwezekano mkubwa Aziz Ki akajiunga na moja ya timu hizo pale msimu utakapofika tamati huku ikielezwa uongozi wa Yanga tayari umeanza mchakato wa kusaka mbadala wake

Yanga inahusishwa kumrejesha kiungo mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto', mazungumzo yakielezwa kuwa katika hatua za mwisho

Hivi karibuni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisikika akitamba na kuwataarifa Azam Fc kuwa wajiandae kwani kuna pigo linakwenda kuwakumba pale dirisha litakapofunguliwa!

Aziz Ki amekuwa nguzo ya mafanikio ya Yanga katika misimu mitatu aliyowatumikia Wananchi akitwaa mataji mawili ya ligi kuu ya NBC, FA, kucheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) na robo fainali ya ligi ya mabingwa (CAF CL)

Msimu uliopita ulikuwa wa mafanikio zaidi kwake akibeba tuzo ya mchezaji bora (MVP), kiungo bora na mfungaji bora akifunga mabao 21

Msimu huu amefunga mabao 9 huku pia akitoa assist 8 akihusika katika mabao 17 yaliyofungwa na Yanga kwenye ligi

Maumivu ya yanayojirudia ya mgongo na nyonga ni wazi yamechangia kumpunguza kasi msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
44m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’