Yanga yaanza hesabu za Kimataifa 2025/26

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2025
Yanga yaanza hesabu za Kimataifa 2025/26

Wakati msimu wa ligi kuu 2024/25 ukielekea ukingoni, Yanga tayari inayo tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) 2025/26

Alama 70 kileleni mwa msimamo wa ligi, Yanga imejihakikishia kumaliza msimu katika nafasi mbili za juu naa hivyo moja kwa moja kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe, amefichua kuwa baada ya kile kilichotokea msimu huu, wameanza michakato ya maboresho ya kikosi mapema ili kuhakikisha msimu ujao wanakuwa na timu bora itakayofanya vizuri zaidi

Kamwe amesema hatua ya kwanza uongozi unafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi kwa kuwaongezea mikataba wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni lakini wako katika mipango ya Mwalimu

Lakini pia tayari maskauti wako sokoni kusaka wachezaji wapya ambao watasajiliwa

"Tumeanza kuboresha timu yetu kwa ajili ya msimu ujao, maboresho ya kwanza ni kubakisha nyota tulionao kwa mujibu wa ripoti ya mwalimu, wale ambao watataka kuondoka, tutaangalia kwa maslahi ya klabu nani tumuondoe, lakini malengo makubwa ni kutengeneza timu ya msimu ujao kwa sababu tayari tuna tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa"

"Wachezaji bora wengi lazima uanze kuwatafuta mapema, kama mchezaji yupo huru maana yake mkataba wake unaelekea kumalizika na yule mwenye mkataba mazungumzo na klabu yake yanaanza kipindi hiki," alisema Kamwe

Baada ya misimu miwili ya kucheza fainali ya CAF CC na robo fainali ya CAF CL, msimu huu Yanga iliishia hatua ya makundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
51m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’