Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akizungumza mbele ya mashabiki baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate hapo jana, aliweka msisitizo kuwa ni mechi tatu tu zilizobaki kuhitimisha msimu huu
Jana iliendeleza ubabe wake katika ligi na kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 70
Injinia Hersi alisema kazi iliyobaki ni kushinda mechi tatu zilizosalia ili kutangaza ubingwa
"Leo tumeshinda mabao 4-0, na zimebaki mechi tatu kumaliza msimu, basi tupambane tushinde mechi zote," alichagiza Hersi mbele ya mashabiki wa Yanga waliokuwa na shamrashamra baada ya ushindi huo mnono
Mechi zilizobaki ni dhidi ya Namungo Fc (KMC Complex - May 13), Prisons (Sokoine Stadium -May 21) na Dodoma Jiji (KMC Complex - May 25)
Yanga iliweka msimamo wa kutocheza mchezo dhidi ya Simba (mechi namba 184) baada ya Simba kuingia mitini katika mchezo uliopaswa kupigwa March 08 wakidai kunyimwa nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa