Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo uliopigwa dimba la Tanzanite Kwaraa, Manyara
Clement Mzize ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo akifunga mabao mawili huku Clatous Chama akifunga bao maridadi kabisa kupitia mpira wa adhabu katika kipindi cha pili
Mzize alifunga bao la uongozi dakika ya 39 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Stephane Aziz Ki na kumshinda mlinda lango John Noble
Aziz Ki akaongeza bao la pili dakika tatu baadae akitumia makosa ya mlinda lango Noble
Yanga iliendelea kutawala mchezo katika kipindi cha pili na kuongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Mzize na Chama
Mzize amesogea juu katika mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 13 akiendelea kuweka rekodi ya aina yake msimu huu
Yanga imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha alama 70 ambapo sasa ni alama 13 mbele ya watani zao Simba wanaoshika nafasi ya pili