Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako Babati, Manyara kumenyana na Fountain Gate
Mechi nyingine muhimu kwa Wananchi kuendelea kusogea karibu na ubingwa wa 31 ligi kuu
Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakikusanya alama 67, wananchi wanapambania alama 12 za mechi nne zilizosalia
Kama watashinda leo watajiweka katika nafasi nzuri kwani zitabaki mechi tatu, mbili zikiwa nyumbani na moja ugenini
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema wanakwenda katika mchezo huo wakifahamu wanahitaji kupambana ili kuibuka na ushindi
Hamdi amethiitisha wachezaji Pacome Zouzoua na Khalid Aucho watakosekana huku baadhi ya wachezaji kama Kennedy Musonda na Stephane Aziz Ki nao wakiwa hawako fit kwa asilimia 100 lakini wanaweza kutumika katika mchezo huo
Timu hizo zilipokutana katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 hivyo leo Wananchi wanatarajia timu yao kuendeleza ubabe