Zikiwa zimesalia siku tatu kuelekea mchezo wa ligi kuu kati ya Fountain Gate dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumatatu, April 21 katika uwanja Tanzanite Kwaaraa huko Manyara, wenyeji wa mchezo huo wameanza tambo mapemaaa
Kupitia kurasa rasmi za Fountain Gate katika mitandao ya kijamii, wameweka machapisho mbalimbali yenye tambo na 'kero' dhidi ya wapinzani wao Yanga
Aidha Fountain Gate tayari wametangaza viingilio vya mchezo huo, kiingilio cha juu kikiwa Tsh 100,000/- kwa tiketi za VVIP
VIP A ni Tsh 30,000/- na VIP B ni Tsh 20,000/- Tanzanite ikiwa Tsh 10,000/-
Ni kama Fountain Gate wanachokoza ugemvi kwa bingwa mtetezi, sasa wanapaswa kuhakikisha wananguvu ya kupigana...!
Katika mchezo wa raundi ya kwanza, walikubali kichapo cha mabao 5-0 dimba la KMC Complex
Ni juzi tu Yanga imetoka kushusha kipigo cha mabao 8-1 dhidi ya Stand United mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB
Stand walikata tiketi ya kutinga robo fainali kwa ushindi dhidi ya Fountain Gate mchezo ukipigwa hapohapo Tanzanite Kwaraa
Kabla ya Stand kuwakabili Yanga, msemaji wao alimuomba kocha Miloud Hamdi kupanga kikosi chake bora huku akitamba wangeibuka na ushindi...!
Yanga inaendelea na maandalizi ya mchezo huo jijini Dar es salaam ambapo kikosi kitaondoka kesho Jumamosi, April 19 kuelekea Manyara