Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi huenda asionekane tena kikosini msimu huu kutokana na changamoto ya majeraha yake
Yao alianza mazoezi mepesi lakini imebainika bado hajapona jeraha lake sawasawa na atahitaji muda zaidi wa matibabu
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema madaktari wameshauri nyota huyo raia wa Ivory Coast apate muda zaidi wa kupumzika
"Yao bado hajapona sawasawa na pengine tunaweza tusimuone tena uwanjani msimu huu. Imeshauriwa apewe muda zaidi wa mapumziko na kuendelea kuimarika maana imeonekana kama atarejeshwa uwanjani haraka inaweza kumsababishia madhara zaidi," alisema Kamwe
Akizungumzia hali ya majeruhi wengine Pacome Zouzoua na Khalid Aucho, msemaji huyo wa Yanga amesema Aucho ataendelea kuwa nje kwa wiki mbili zaidi hivyo atakosa mechi ya ligi kuu dhidi ya Fountain Gate itakayopigwa April 21 pamoja na michuano ya ligi ya muungano
Pacome atajumuishwa katika kikosi kitakachoelekea mkoani Manyara kuikabili Fountain Gate lakini hatacheza mchezo huo
Kamwe amesema, kwa kutegemea maendeleo yake, anaweza kushiriki mechi ya fainali ya ligi ya Muungano kama Yanga itavuka hatua ya robo na nusu fainali