Leo mchezo wa nne wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB utakamilishwa kwa mabingwa watetezi Yanga kumenyana na Stand United katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex
Klabu za JKT Tanzania, Singida BS na Simba tayari zimekata tiketi ya nusu fainali hivyo mshindi wa mchezo wa leo ataungana na timu hizo
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi licha ya kuwa utakutanisha timu za madaraja tofauti
Yanga ambao ni mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu ya NBC, wanakutana na Stand United inayoshika nafasi ya tatu katika ligi ya Championship
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema wanauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa na lengo ni kushinda ili wasonge mbele katika hatua inayofuata
Mshindi wa mchezo huo atakutana na JKT Tanzania katika nusu fainali