Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi jana aliendelea kudhihirisha kwa nini Yanga haikujiuliza mara mbili kumuajiri baada ya kuondoka ghafla kocha Sead Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad
Ukiwa ni mchezo wake wa 10 tangu aanze kuinoa Yanga, Hamdi aliwaongoza Wananchi kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Azam Fc na kuendelea kuiweka Yanga katika nafazi nzuri ya kutetea ubingwa
Hamdi sasa ameiongoza Yanga kushinda mechi 9 mfululizo katika ligi na kombe la Shirikisho la CRDB
Ilikuwa February 10 2025 alipoanza rasmi majukumu yake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Baada ya mchezo huo, Yanga haijapoteza mchezo mwingine wowote katika mechi 9 zilizofuata
Ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC, Singida BS(2-1), Mashujaa Fc (5-0), Pamba Fc (3-0), Coastal Union (3-1), Songea United (2-0), Tabora United (3-0), Coastal Union (1-0) na Azam Fc (2-1)
Katika mechi 10 alizoiongoza Yanga mpaka sasa, Wananchi wamepachika mabao 27 huku wakiruhusu mabao manne tu