Juzi Yanga ilipata ushindi muhimu wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
Ilikuwa ni mechi ambayo ilitengenezewa presha kubwa nje ya uwanjani lakini presha hiyo haikuathiri ubora wa Wananchi ndani ya uwanja
Baadhi ya wachezaji wa Tabora United walionekana kukamia mchezo wakiongozwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga Heritier Makambo ambaye mara kadhaa aliingia kwenye mzozo wa beki kisiki wa Yanga Ibrahim Bacca

Ni kama Makambo alikuwa na ahadi nyingine ya bonus nje ya ile Milioni 60 iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Paul Chacha kwa timu hiyo kama ingeshinda mchezo dhidi ya Yanga
Makambo hakufurukuta mbele ya nahodha Dickson Job na Bacca, hakuweza kupiga shuti lolote langoni kwa Yanga

Bacca na Job wameendelea kudhihirisha kwa sasa ndio mabeki bora pacha yao ikitamba kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' pia
Msimu huu Yanga imepoteza mchezo mmoja tu, ambao wawili hao walianza pamoja kikosi cha kwanza
Ulikuwa mchezo dhidi ya Azam Fc ambao hata hivyo Bacca alitolewa nje kwa kadi nyekundu
Hawa ndio kiboko ya washambuliaji wanaokamia Mechi...!