Ridhiwani akana kuutaka Uwenyekiti Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2018
Ridhiwani akana kuutaka Uwenyekiti Yanga
Mwezi ujao Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wake ambayo sasa ina Kaimiwa na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga tangu kujiuzulu kwa Yusufu Manji.

Jina la Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete limekuwa likitajwa kuwa miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi katika klabu ya Yanga.

Ridhiwani mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mh Jakaya Kikwete, amekata mzizi wa fitina kwa kusema hana mpango wa kuwania nafasi hiyo.

Ridhiwani amekiri kushawishiwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kumtaka ugombee nafasi hiyo lakini mwenyewe amesema licha ya kubanwa na majukumu ya Kiserikali, lakini pia hana sifa za kugombea nafasi hiyo.

"Mimi sio mwanachama wa Yanga, na hiyo ndiyo sifa kuu inayotakiwa ili kuweza kugombea nafasi ya uongozi katika klabu ya Yanga," amesema.

Mwaka 2014 wakati Ridhiwani akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo la Mafia aliwahi kutuhumiwa na uongozi wa Yanga kuwa hakuwa Mwanachama baada ya kushindwa kulipia ada ya uanachama kwa miezi sita mfululizo.

Ridhiwani alikuwa miongoni mwa Wanachama waliokuwa wakipinga hatua ya Bodi ya Wadhamini ya Yanga kumuongezea mwaka mmoja aliyekuwa Mwenyekiti Yusufu Manji.

"Niliwahi kutuhumiwa kuwa mimi sio Mwanachama wa Yanga na hivyo sina Mamlaka ya kuzungumza jambo lolote linaloihusu klabu ya Yanga," amesema.

"Sasa leo napata wapi nguvu ya kugombea nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi?," amehoji Ridhiwani
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’