Matchday : Tabora United vs Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2025
Matchday : Tabora United vs Yanga, NBC PL

Baada ya mapumziko ya takribani wiki tatu, mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inarejea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako mkoani Tabora kuikabili Tabora United

Ni mechi iliyozungumzwa zaidi, vita ya maneno ikisikika nje ya uwanja kila timu ikijinasibu kuibuka na ushindi

Yanga ilitua Tabora jana na jioni vijana wa Miloud Hamdi wakafanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Wananchi wamepania kushinda mchezo huo ili kulipa kisasi baada ya kupoteza mechi ya duru ya kwanza kwa kufungwa mabao 3-1

Mji wa Tabora kwa siku mbili umezizima kwa shangwe la mashabiki wa Yanga, ni wazi leo uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hautatosha kwa wingi wa mashabiki ambao wanatarajiwa kujitokeza

Licha ya Yanga kuwa ugenini, ndio inayoonekana kama iko nyumbani huku wenyeji wakikerwa na ufalme huo unao-onyeshwa na Wananchi

Mchezo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’