Winga wa Yanga Simon Msuva amekamilisha usajili kwenye klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Msuva alitua nchini Morocco juzi, ambapo jana alifanyiwa vipimo vya Afya na kufuzu.
Sasa Rasmi Msuva ni mchezaji wa Difaa.
Klabu ya Yanga inatarajiwa kutuma vibali vyake muhimu kwa klabu hiyo ili aanze maisha mapya ya soka nchini Morocco.
Difaa ilikubaliana na Yanga kutoa kwanza asilimia 80 ya ada ya uhamisho wa Msuva kabla ya vipimo vya Afya kisha kumalizia asilimia 20 pale Yanga itakapokamilisha kutuma vibali vyake.

ADVERTISE HERE