Wananchi Bukoba waunga mkono msimamo Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Mar 2025
Wananchi Bukoba waunga mkono msimamo Yanga

Viongozi, wanachama na mashabiki wa timu ya Yanga Tawi la Bukoba mkoani Kagera wamekutana kuunga mkono kauli ya Kamati ya Utendaji ya timu hiyo kuwa hawatacheza tena mechi dhidi ya Simba

Mchezo huo wa Ligi Kuu namba 184 ulipaswa kuchezwa Machi 8, 2025 lakini haukufanyika kutokana na Simba kugomea baada ya taarifa ya kuzuiwa kufanya mazoezi na mabaunsa wa Yanga siku moja kabla ya mechi uwanja wa Mkapa

Katibu wa Matawi ya Yanga mkoani Kagera Jamali Kalumuna aliwaongoza wadau kufungua kikao cha kutoa kauli ya pamoja kuwa hawataki tena mchezo wa marudiano badala yake wanaiomba Bodi ya Ligi Kuu na TFF kuwapatia Yanga pointi 3 na goli 3 kwa mujibu wa kanuni

"Kwanza kabisa tunaungana na kamati tendaji kupitia kwa Rais wa Yanga injinia Hersi kuwa kwa pamoja matawi yote ya Mkoa wa Kagera hatutacheza tunachohitaji ni kupatiwa pointi zetu na magoli yetu matatu kwa sababu kuahirishwa kwa mchezo huo hakukufata kanuni,"amesema Kalumuna

Peter Matete, Mjumbe wa Tawi la Yanga Bukoba amesema ni vyema kanuni zikazingatiwa ambapo ameongeza kuwa sio salama kwa maswala ya mpira kufuata busara na kushauri kuwa timu yoyote isipofuata kanuni bila kujali ukubwa wa Timu ikatwe point na hiyo itasaidia kuweka heshima ya mpira nchini na kupandisha hadhi ya ligi ya Tanzania

Ezra Festo mwanachama wa Yanga mkoani Kagera amesema kuwa ni aibu na kukosa kuwajibika endapo busara zinaendekezwa na kufuta kanuni za ligi na kuumiza hisia za watanzania ambao ndio wadau wakubwa wa mpira wa miguu huku akidai kuwa kwa mara ya kwanza viongozi wa Bodi ya Ligi wanapaswa kuwajibika kwa kuumiza hisia za mashabiki walitoka ndani ya nchi na nje ya nchi kuja kushuhudia mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’