Mabingwa watetezi kombe la Shirikisho la CRDB, Yanga imetinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Songea United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Mabao ya Duke Abuya na Jonathan Ikangalombo yaliyotokana na pasi za Pacome Zouzoua yalitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo muhimu
Yanga ilitawala mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi hasa katika kipindi cha kwanza lakini umakini mdogo katika umaliziaji na uimara wa mlinda lango wa Songea United alikuwa kikwazo kwa Yanga kupata ushindi mnono zaidi
Ni ushindi wa 21 mfululizo kwa Yanga katika michuano ya kombe la FA, Wananchi wakiendelea kuweka rekodi ya aina yake
ADVERTISE HERE