Yanga kutangaza utalii Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2025
Yanga kutangaza utalii Zanzibar

Klabu ya Yanga leo imeingia ushirikiano na Kamisheni ya Utalii chini ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa ajili ya kutangaza vivutio vya Utalii visiwani Zanzibar

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mahusiano hayo yatadumu hadi mwisho wa msimu 2025/26 ambapo klabu ya Yanga itaendelea kuvaa nembo ya Visit Zanzibar katika mashindano yote

"Tunafuraha kubwa kupata fursa hii ya kuingia mahusiano ya ushirikiano na Kamisheni ya Utalii chini ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa ajili ya kutangaza vivutio vya Utalii hapa Zanzibar"

"Mahusiano haya yatadumu mpaka mwisho wa msimu wa 2025/26. Logo ya 'Visit Zanzibar' itaendelea kubaki kwenye jezi yetu katika michuano yote tutakayoshiriki"

"Yanga tunaitazama Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kama jicho la Zanzibar, mahusiano tunayoingia leo ni kwa ajili ya kuutangaza utalii wa Zanzibar kupitia Klabu yetu. Na mahusiano haya sio kutangaza tu bali kutoa elimu na uelewa juu ya vivutio vyote vya utalii Zanzibar"

"Huna haja ya kwenda Ibiza au Dubai kufanya utalii wakati Zanzibar ipo, kwanini upeleke hela yako nje ya nchi wakati Zanzibar yetu imebarikiwa vivutio vingi vya utalii? Klabu yetu inakwenda kuweka nguvu kuongeza idadi kubwa ya watalii wa ndani na nje watakaokuja kuitembelea Zanzibar," amesema Hersi

Naye Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga ameipongeza klabu ya Yanga chini ya Rais Hersi Said kwa ushiriano ambao wameendelea kutoa na hatimaye kufanikisha kusainiwa kwa makubaliano hayo leo

"Niwapongeze sana Viongozi wa Yanga chini ya Rais wake Eng.Hersi Said kwa ushirikiano mkubwa mlioutoa kutoka mwanzo mpaka leo tunapokwenda kusaini mahusiano haya ya ushirikiano wa kutangaza Utalii wa Zanzibar"

"Sekta ya Utalii ina ushindani mkubwa sana, licha ya jina kubwa tulilokuwa nalo bado tunapata ushindani sana kutoka katika Visiwa vya jirani hivyo ni lazima kama Wizara tuweke nguvu kubwa kwenye kujitangaza"

"Niseme wazi kama kuna taasisi bora yenye nguvu na ushawishi ambayo tungeweza kufanya nayo kazi kutusaidia kwenye suala hili la kutangaza vivutio vyetu vya Utalii hapa Zanzibar, basi namba moja na sahihi kwa sasa ni Yanga," alisema Sogara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’