Tabora United vs Yanga, hii ni mechi ya kisasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2025
Tabora United vs Yanga, hii ni mechi ya kisasi

Jumanne ijayo April 1 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga watakuwa dimbani kuikabili Tabora United katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC

Yanga itaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya matokeo ya mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Yanga kukubali kipigo cha mabao 3-1

Ni mechi ya kisasi kwa Wananchi, Tabora United ni moja ya timu mbili zilizotibua rekodi ya Yanga msimu huu. Walina asali hao kutoka Tabora na Azam Fc walitibua rekodi nzuri ambayo Yanga walianza nayo msimu kwa kushinda mechi nane mfululizo

Baada ya kupoteza mechi hizo mbili, unaweza kusema Wananchi walitoka kwenye reli kwani ilipelekea aliyekuwa Kocha Mkuu Miguel Gamondi akatimuliwa na kumleta kocha mpya Sead Ramovic ambaye nae akapoteza mechi mbili muhimu za ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal na MC Alger

Hivyo ni wazi Wananchi wanauendelea mchezo dhidi ya Tabora United wakikumbuka madhira waliyokumbana nayo baada ya kupoteza mchezo wa duru ya kwanza dhidi yao

Katika kipindi hiki ambacho ligi inaelekea ukingoni, kila mchezo ni kama fainali hakuna nafasi ya kudondosha alama katika mechi 7 zilizobaki

Yanga itakwenda Tabora baada ya mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Songea United utakaopigwa Jumamosi, March 29 uwanja wa KMC Complex

Wananchi wakati huo watakuwa na full-squad kwani wachezaji waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa watakuwa wmerejea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’