Majira ya saa 10 jioni leo uwanja wa Airtel unaomilikiwa na Singida Black utazinduliwa kwa mchezo wa kirafiki kati ya wenyeji Singida Black Stars dhidi ya Yanga
Kikosi cha Yanga kitua Singida jana tayari kushiriki tukio hilo la kihistoria kwa wakazi wa mkoa wa Singida na maeneo ya jirani
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Hamis Mwinjuma anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo
Licha ya kuwa ni mechi ya kirafiki lakini kila timu imejipanga kuwapa furaha mashabiki wake
Wakati Singida Black Stars wakitamba kulinda heshima ya tukio kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga, Wananchi wamepania kutibua furaha ya wenyeji wao
Ni mechi ambayo itampa nafasi kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi kuwatumia wachezaji ambao hawakutumika sana msimu huu
Yanga inawakosa wachezaji 10 ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa
Hivyo ni mechi ambayo wachezaji kama Denis Nkane, Jonas Mkude, Aziz Andabwile, Kibwana Shomari na hata mlinda lango Aboubakar Khomein anaweza kuonekana dimbani