Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa mlinda lango wa Yanga Aboubakar Khomein
Khomein aliyetua Yanga msimu huu akitokea klabu ya Ihefu Fc (sasa Singida Black Stars) alianza vyema majukumu yake na Wananchi akitumika kama kipa mbadala wa Djigui Diarra
Hata hivyo akapoteza nafasi yake baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc uliopigwa dimba la KMC Complex Yanga ikishinda mabao 3-2
Mabao mawili 'mapesi' aliyoruhusu katika mchezo huo pengine ndio yaliyomfanya apoteze nafasi yake mbele ya Aboutwalib Mshery
Hiyo ndio presha ya kucheza timu kubwa kama Yanga.Bila shaka Khomein amepata muda wa kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana katika mchezo huo na pengine anachosubiri ni wito tu wa benchi la ufundi ili kurejea katika kikosi cha kwanza
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa
HAPPY BIRTHDAY KHOMEIN...!