Baada ya mapumziko ya takribani siku 6, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini leo kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata
March 24 Yanga itashiriki tukio la uzinduzi wa uwanja wa Singida Black Stars ambapo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya walima alizeti hao
March 29 Yanga itarudi KMC Complex kumenyana na Songea United katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB
Baada ya mchezo huo Yanga itasafiri mkoani Tabora kuikabili Tabora United katika mchezo wa raundi ya 23 ligi kuu ya NBC utakaopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi April 1 2025
ADVERTISE HERE