Baada ya Bodi ya Ligi(TPLB) kudai tuhuma za rushwa ni moja ya sababu zilizopelekea kuahirisha mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi ndio inayohusika masuala ya uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa, haina taarifa ya uwepo wa tuhuma hizo
Akihojiwa na chombo kimoja cha habari mapema leo, Holle Makungu ambaye ni Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Temeke, amesema hakukuwa na taarifa yoyote kuwa rushwa imehusika katika mchezo huo
"Hatujaanzisha uchunguzi kwa kuwa hakukuwa na taarifa yoyote kuwa rushwa imehusika katika mchezo huo"
"Kwa mujibu wa Sheria na Mamlaka za nchi, chombo ambacho kinahusu uchunguzi wa masuala ya rushwa ni TAKUKURU ila kama ni migogoro tu ya watu kutozingatia kanuni za michezo, basi hayo ni mambo ya vyombo vya michezo," alisma Makungu