Mwandila, Nsajigwa hawajaipa Yanga ushindi tangu Lwandamina aondoke

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2018
Mwandila, Nsajigwa hawajaipa Yanga ushindi tangu Lwandamina aondoke
Tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina, mabingwa hao wa kihistoria wa soka la Tanzania hawajaonja radha ya ushindi.

Mchezo wa mwisho wa Yanga kushinda ilikuwa April 07 ilipoichapa Wolaitta Dicha mabao 2-0 kwenye uwanja wa Taifa.

Huo ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Lwandamina kukaa kwenye benchi la Ufundi la Yanga kabla hajatimkia ZESCO siku mbili baadae.

Baada ya ushindi huo, Yanga haijaonja tena radha ya ushindi katika michezo mitano iliyocheza bila Lwandamina.

April 11 ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United kabla ya kuchapwa bao 1-0 na Wolaitta Dicha April 18.

Ikaja ikalazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City April 22 kabla ya kuchapwa bao 1-0 na Simba April 29.

Juzi imechapwa mabao 4-0 na USM Alger kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Makocha Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa wameshindwa kuipa Yanga ushindi tangu wakabidhiwe mikoba ya Lwandamina.

Aidha kocha mpya Mwinyi Zahera ambaye hata hivyo bado hajapata vibali vya kufanya kazi nchini naye anasaka ushindi wake wa kwanza akiwa na kikosi cha Yanga.

Yanga itakuwa na michezo miwili ya ligi (May 10 dhidi ya Prisons, May 13 dhidi ya Mtibwa Sugar) kabla haijarejea jijini Dar es salaam kuikabili Rayon Sports kwenye mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’