Jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliweka hadharani ratiba ya mechi za hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB ambapo Yanga itashuka dimbani March 29 kumenyana na Songea United
Mchezo huo wa kuwania tiketi ya kutinga robo fainali utapigwa uwanja wa KMC Complex
Baada ya mchezo Wananchi watakuwa na siku mbili za mapumziko kabla ya kuikabili Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao umepangwa kupigwa April 1 2025
Bado haijafahamika mchezo dhidi ya Tabora United utapigwa uwanja gani kwani dimba la Ali Hassan Mwinyi na hata CCM Kirumba ambako Tabora walicheza meechi yao iliyopita vimefungiwa na Bodi ya Ligi
ADVERTISE HERE