Hii kesi ya Dabi itakwenda kumalizwa na FIFA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2025
Hii kesi ya Dabi itakwenda kumalizwa na FIFA

Baada ya kutimiza taratibu zote za mchezo dhidi ya Simba ambao ulipaswa kupigwa jana saa 1:15 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga imeweka msimamo kuwa hawatakuwa tayari kucheza mechi nyingine yoyote dhidi dhidi ya Simba kwenye ligi msimu huu kufuatia kitendo cha bodi ya ligi kuahirisha mchezo huo pasipo sababu za msingi

Andiko la Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji limefunga mjadala juu ya msimamo wa Yanga kuwa mechi ya Derby imemalizika March 08 na sasa Yanga inawekeza nguvu zake katika ratiba nyingine na haitakuwa tayari kurudishwa nyuma

Nini kitatokea?

Kwa kuwa Bodi ya Ligi imeonyesha waziwazi kuchagua upande pasipo kujali maslahi ya wadau wengine, wataendelea na kile walichopanga

Watapanga tarehe ya mechi nyingine, Yanga haitatokea kucheza mechi hiyo, hivyo wataipa Simba alama tatu wadadisi wa mambo wakiamini hapa ndipo lililopo lengo kuu la vurugu zilizoanzishwa juzi usiku pale uwanja wa Benjamin Mkapa

Lakini jambo la uhakika haki ya Yanga haitapotea, kesi hili itakwenda kumalizwa na mamlaka za juu za usimamizi wa soka duniani, FIFA

Pasipo na shaka Yanga watapewa haki yao kwani walichofanya Bodi ya ligi kuahirisha mechi kinyume na kanuni ni kama wamejichimbia kaburi

Hakuna kanuni ambayo inahalalisha timu moja kugomea mchezo eti kwa kuwa hawajapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa mechi

Kama kuna makosa yalifanyika kupelekea wao kushindwa kufanya mazoezi kanuni ziko wazi adhabu ilipaswa kutolewa kwa kuzingatia kanuni

Kuamua kutocheza mechi ni kosa pia ambalo linapaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni kwani kosa moja halihalalishi kosa jingine

Bodi ya ligi wenyewe wamekiri klabu ya Simba haikutoa taarifa kwa timu mwenyeji wala wamiliki wa uwanja juu ya kusudio lao la kwenda kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa muda huo wa usiku

Aidha Kamati iliyotoa maamuzi ya kuahirisha mchezo huo haina nguvu kisheria, tangu lini kamati ya saa 72 ikajadili mchezo ambao haujachezwa?

Kamati hiyo pia haina mamlaka ya kuchunguza mambo yanayohusiana na vurugu kwa sababu hayo ni masuala yenye jinai ndani yake ambayo yanapaswa kushughulikiwa na mamlaka husika

Kwa ujumla tamko la Bodi ya Ligi ni kama kisu ambacho wamejiwekea wenyewe shingoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’