Yanga ilizuiwa kufanya mazoezi kwa Mkapa mechi ya Oktoba 19

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2025
Yanga ilizuiwa kufanya mazoezi kwa Mkapa mechi ya Oktoba 19

Klabu ya Simba imetishia haitapeleka timu uwanjani katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao umepangwa kupigwa baadae leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imedai maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi katika dimba la Mkapa siku moja kabla ya mechi

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amesema katika mechi iliyopita Oktoba 19 Yanga ilizuiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi kama ilivyotokea kwa Simba licha ya kuwa kanuni inawaruhusu

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Simon ameandika ujumbe huu

"Kwa mujibu wa kanuni, ni kweli kwamba timu ngeni ina haki ya kufanya mazoezi angalau mara moja kabla ya mechi.

Hata hivyo, kwa kuwa ligi yetu inaendeshwa kwa busara, na ikizingatiwa kuwa katika mzunguko wa kwanza Klabu ya Yanga ilinyimwa haki ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi, basi hakuna uhalali wa kuruhusu wenzetu kufanya mazoezi ili kuepuka upendeleo wa aina yoyote (“double standard”).

Kama mamlaka zingekuwa makini katika kusimamia kanuni kwa kiwango sawa na wanavyofanya katika kutoa faini kwa vilabu na kuwafungia wasemaji, hali hii isingekuwepo.

NB: Fanyeni yote Afrika nzima inasubiria derby ya Kariakoo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’