Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki anaweza kutumika katika mechi dhidi ya Simba itakayopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa licha ya changamoto aliyopata katika mchezo uliopita
Aziz Ki alipata changamoto ya nyonga katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Hamdi amesema hatma yake itafahamika hapo kesho
"Niwe mkweli, tuna mchezaji mmoja Aziz Ki ambaye ana shida kidogo. Matarajio yetu ataweza kucheza mechi dhidi ya Simba lakini hilo litafahamika hapo kesho," alisema Hamdi
Jioni ya leo Yanga itakamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo huo, pengine baada ya mazoezi hayo, hatma ya MVP huyo wa ligi kuu msimu uliopita itafahamika
ADVERTISE HERE