Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki
Akiwa katika msimu wake wa tatu na Yanga, Aziz Ki ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga
Msimu uliopita ulikuwa wa mafanikio zaidi kwake akibeba tuzo tatu muhimu za ligi kuu ya NBC yaani MVP, mfungaji bora na kiungo bora
Alianza msimu huu taratibu lakini unaweza kusema tayari amerejea katika kiwango chake
Wakati huu Aziz Ki yuko Avic Town na wachezaji wengine wakiendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii muhimu ya kumbukumbu ya kuzaliwa
HAPPY BIRTHDAY AZIZ KI...!
ADVERTISE HERE