Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, March 08 yanakwenda vizuri
Kamwe amesema kikosi kilirejea mazoezini jana baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, watakuwa na muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo ambao kwa sasa umetawala kila kona
"Niwaambie mashabiki na wanachama wa Yanga, tayari tumeanza maandalizi kuelekea mchezo huu, wachezaji wetu wameingia kambini kukamilisha maandalizi ya siku hii ya tarehe 8 kuwakabili Simba"
"Tuna rekodi nzuri dhidi ya Simba, tumeshinda mara nne mfululizo lakin tunatambua hiyo rekodi nzuri ndio imeongeza ugumu wa mchezo kwani wenzetu watakuja wakitaka kupambana kufuta uteja"
"Sisi tunajiandaa na hilo na tuko tayari kupambana nao na kwa kuzingatia maandalizi ambayo tunafanya, ubora wa tmu yetu na sapoti tunayopata kutoka kwa Wanachama na mashabiki wa Yanga, tutakwenda kupambana na kupata matokeo mazuri March 08, " alisema Kamwe
Kamwe amesisitiza malengo ya Yanga ni kushinda mchezo huo ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi akiamini bado watakuwa na kazi ya kupambana katika mechi 7 zitakazosalia ili kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo