Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga tayari wako jijini Mwanza siku mbili kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa uwanja wa CCM Kirumba, Ijumaa Februari 28
Utakuwa mchezo wa raundi ya 22, alama tatu za mchezo huo zitazidi kuisogeza Yanga karibu na mkakati wake wa kutetea taji la Ligi Kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Msimu huu ushindani ni mkali kulinganisha na misimu iliyopita ambayo nyakati kama hizi Yanga iliongoza juu ya msimamo kwa tofauti ya alama nyingi lakini sasa ni nne tu
Na hii ndio sababu inayofanya kila mchezo kuwa na umuhimu wa kipekee, hakuna nafasi ya kudondosha alama kwani kufanya hivyo ni kuvuruga hesabu katika mbio za ubingwa
ADVERTISE HERE