Juzi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc, kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua alikuwa chachu ya ushindi wa mabao 5-0 akitoa pasi mbili na kuonyesha kiwango bora ambacho kilimfanya achaguliwe nyota wa mchezo huo
Pacome amewashukuru mashabiki wa Yanga mkoani Kigoma ambao waliwapa hamasa kubwa tangu walipotua mkoani humo na pia wakajitokeza kwa wingi uwanja wa Lake Tanganyika kuwashangilia
"Tulipata mapokezi ya aina yake Kigoma, kwa kweli tunawashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi tangu tumewasili Kigoma na hata kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo"
"Sapoti hii ya mashabiki ni muhimu sana wakati huu tukielekea katika mechi za kuhitimisha msimu"
"Kila mchezo kwetu ni muhimu na hakuna muda wakupoteza, tunajua ushindani ni mkubwa nasi tunapambana kuwa bora kupata matokeo uwanjani," alisema Pacome
Pacome ameendelea kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu huu akihusika katika mabao 13 akifunga 7 na kutoa assist 6
Ameifikia rekodi yake ya mabao 7 ya msimu uliopita huku akiwa ameipita rekodi yake ya asisti 5 msimu uliopita