Hakuna tena nafasi ya makosa, kila mechi alama 3

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Feb 2025
Hakuna tena nafasi ya makosa, kila mechi alama 3

Baada ya Simba kudondosha alama mbele ya Azam Fc jana kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2, Yanga imejihakikishia kukaa juu ya kilele cha msimamo wa ligi

Alama 55 kileleni baada ya mechi 21 huku watani zao Simba wakiwa nafasi ya pili na alama 51 pamoja na mechi moja ya kiporo

Yanga sasa imeshikilia hatma yake katika mbio za ubingwa, ushindi katika kila mechi utawahakikishia Wananchi kurejesha ubingwa Jangwani kwa msimu wa nne mfululizo

Kikosi cha kocha Miloud Hamdi sasa hakipaswi kutoa tena nafasi kwa watani zao kurudi juu ya msimamo kwani hilo litatokea endapo Yanga itafanya makosa

Ijumaa ya wiki hii Yanga itakuwa Mwanza kumenyana na Pamba Jiji katika mchezo ambao ushindi ndio matokeo pekee ambayo Wananchi watahitaji

Kama Yanga itashinda mechi ijayo, maana yake ni kuwa itakwenda katika mchezo wa Derby dhidi ya Simba ikiwa haiko katika presha kubwa kwani hata matokeo ya sare yatawahakikishia kuendelea kubaki kileleni

Ni mechi 9 tu zimesalia kuhitimisha msimu huu, hizi ni fainali 9 ambazo Wananchi wanahitaji alama 27

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’