Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa wa KMC Complex
Yanga ilikuwa na kipindi cha kwanza bora ikifunga magoli yake kupitia washambuliaji vinara Clement Mzize na Prince Dube
Kipindi cha pili Singida BS walichukua mchezo na kuipa Yanga changamoto hasa kupitia mashambulizi ya kushitukiza
Hata hivyo Yanga ilitengeneza nafasi kadhaa kipindi cha pili lakini Pacome Zouzoua hakuweza kuweka mpira kambani katika moja ya nafasi adimu
Dakika za lala salama Jonathan Sowah alitumia makosa ya Djigui Diarra aliyetema krosi ya Edmund John kufunga bao pekee la Singida BS
Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amewapongeza wachezaji wake kwa kushinda mchezo huo
Hamdi amesema kipindi cha pili vijana wake 'walikata moto' kutokana na fatique iliyosababishwa na kucheza mechi mfululizo
Baada ya kuikabili KMC Februari 14, leo tena imeshuka dimbani siku tatu tu tangu ipate ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC
Ni alama tatu muhimu ambazo zinaifanya Yanga ifikishe alama 52 na kujiimarisha juu ya msimamo