Aziz Ki amelipa mahari huko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2025
Aziz Ki amelipa mahari huko

Mwanamitindo Hamisa Mobetto leo Februari 15, 2025, amelipiwa mahari ya ng'ombe 30 na mume wake mtarajiwa, Stephanie Aziz Ki ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Yanga SC raia wa Burkina Faso huku mipango kabambe ya ndoa ikiendelea

Mahari hiyo imekabidhiwa na Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said kwa niaba ya familia ya Aziz Ki katika zoezi lililofanyika Viwanja vya Gofu, Mikocheni jijini Dar

Katika zoezi la utoaji wa mahari hiyo, Aziz Ki ameongozana na baadhi ya wachezaji wa Yanga akiwemo Pacome Zouzoua, Bakari Mwamnyeto, Yao Kouassi na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe

Kwa upande wa Hamisa Mobetto, aliingia eneo la tukio akiwa na meneja wake, Paul Mangoma huku warembo 15 wakitangulia wakiwa wamevaa sare

Hamisa Mobetto amesema anamshukuru Mungu kumpata mtu anayeona ndiye anamfaa katika maisha yake na tayari sasa ni mchumba rasmi, tena kijana anayempenda kwa dhati

"Sasa hapa ndiyo nimefika kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye mapenzi ya kweli kwangu. Pia nafsi zetu zimeendana, hapa namuomba Mungu anyooshe mambo yaende kama vile tulivyopanga," alisema Hamisa 

Kwa upande wa Aziz Ki, amesema anaamini safari yake ya muda mrefu imefika kwa kuwa amempata mwanamke anayempenda kutoka ndani ya uvungu wa moyo wake

Aziz Ki aliongeza kuwa, kwa upande wake taratibu zote za uchumba amemaliza, kilichobaki anasubiri ndoa tu iliyopangwa kufungwa kesho Jumapili Februari 16, 2025 huku sherehe rasmi ikitarajiwa kufanyika Februari 19 mwaka huu kwenye ukumbi wa The SuperDome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’